1:56 AM
JINSI MISINGI YA VIZAZI INAVYOWEZA KUKAMATA MAISHA YAKO.
Fahamu kwamba misingi ni
chanzo au asili au chimbuko la mtu. Na msingi wako wa vizazi unatokana na ukoo
wako na kabila lako.
Fahamu pia kwamba yule aliyeanzisha
ukoo wenu na kabila lenu ndiye aliye na nguvu sana katika misingi ya vizazi
vinavyoendelea kuzaliwa baada yake. Na kufanikiwa kwa uzao kunategemea msingi
wa uzao kwa yule mwanzilishi kaujenga kwa nani.
1WAKORINTHO 3:10-11
Biblia inasema “ 10
Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi
mwenye hekima, naliuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini kila
mtu na angalie jinsi anavyojenga juu yake. 11 Maana msingi mwingine hakuna mtu
awezaye kuuweka,isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu kristo”
Mwl. Samwel Kibiriti
+255 765 867574
+255 673 784197
+255 785 855785