HISTORIA FUPI YA MWANDISHI:
Mimi kwa jina ni Samwel Kibiriti ni mwalimu wa
Neno la Mungu ambapo Mungu Baba ameniita katika huduma hii tokea mwaka 2008
January ndipo nikaanza kufanya huduma nikiwa katika ofisi hii ya Ualimu, na
kuzifunua siri za Ufalme wa Mungu kwa watu na kuwapatia Maarifa ya kiroho. Na
mkono wa Mungu na Nguvu zake umekuwa ukitenda matendo makuu katikati ya maisha
ya wanadamu.
Ninafundisha katika makongamano makubwa na katika semina mbalimbali za
makanisani, naza vijana. Pia mimi ni mwalimu wa kufundisha
Neno la Mungu katika shule mbalimbali hapa nchini
kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu.
Na tena Mungu amenipatia
nafasi ya kufundisha Neno lake katika
mitandao hii ya kijamii na ambapo nimefanikiwa kusema na maelfu na maelfu
ya watu kupitia mitandao hii.
Niko tayari kufundisha
Semina na kutumika katika kanisa lolote lile na ministry yoyote ile, tena niko
tayari kufika katika shule yoyote ile na kusema na wanafunzi kwa habari za
ufalme wa Mungu na kuomba nao ili kufunguliwa.
Napenda nikukaribishe
kujifunza zaidi kwa habari za Ufalme wa Mungu kupitia mafundisho mbalimbali
ninayofundisha kwenye mitandao ya kijamii.
Ambapo kwa WhatsApp niko na
magroup mawili, Group la CHUO CHA MAARIFA YA KIROHO na group la CHUO CHA BIASHARA, hapa utapata
maarifa mbalimbali ya kiroho kuhusu maisha yako na kuhusu kufanya biashara na
kupata faida, lakini pia niko kwenye magroup mengine mengi ambapo nimeingizwa
nako huko kufundisha Neno la Mungu.
Kwa Facebook ukihitaji
kujifunza masomo yangu utanipata katika ukurasa huu Samwel Kibiritiministry
Pia unaweza kufuatilia na
kujifunza masomo yangu kupitia blogspot hii
www.samwelkibiritiministry.blogspot.com au unaweza tu ukaandika “Chuo cha Maarifa ya
Kiroho”.
Na kupitia Email utanipata
katika Email hii Pastorkibiriti@gmail.com
Kwa mawasiliano nami kwa kuhitaji msaada wa
maombi ya aina yoyote aukuhitaji Ushauri utanipigia katika namba hizi hapa.
Vodacom +255 765 867574.
Tigo +255 673 784197.
Airtel +255 785 855785.
No comments:
Post a Comment