Semina ya siku 30 ( Christ For All People Church- Mbeya ).
KUYASHUGHULIKIA MALANGO YA KIROHO YANAYOGUSA MFUMO WAKO WA MAISHA YA KILA SIKU.
Day 15 ya semina.
Senior Pastor Samwel Kibiriti.
Halleluy mwana wa Mungu karibu katika semina yetu ya siku ya leo ambapo Mungu atatuhudumia.
KUSHUGHULIKIA LANGO LA UUMBAJI WAKO.
Mwanzo 1:26-27; 5:1-2
JINSI YA KUOMBEA LANGO LAKO LA UUMBAJI MBELE ZA MUNGU ( B ).
Katika semina ya jana nilikupatia hatua 2 za kuombea lango lako la uumbaji mbele za Mungu naomba leo nikupatie hatua nyingine za maombi, ninachotamani ni wewe kuingia kwenye maombi ukiwa na ufahamu wa Neno la Mungu kuomba ili Mungu akurudishe katika maisha yako halisi aliyokuandalia wakati alipokuumba.
HATUA YA TATU YA KUOMBA:
( 3 ) Muombe Mungu alisimamishe kusudi lake katika lango lako la Uumbaji.
Zaburi 33:11 Mithali 16:4a Isaya 46:9-10
🟢 Mungu alipokuumba alikuumba kwa kusudi lake lake njema sana na ndani ya kusudi lako ameyaweka maisha yako yote aliyokupangia kuyaishi hapa duniani kwa kipindi cha miaka aliyokupangia hivyo Mungu alikusudia baada ya kukuleta hapa duniani uweze sasa kuyaishi maisha yako yaliyomo ndani ya kusudi lako la uumbaji, lakini sivyo ilivyo kwenye maisha ya wanadamu wengi wanaishi maisha ambayo hata Mungu anahuzunika moyoni mwake kwasababu ni maisha nje ya kusudi lake la kuwaumba.
Unahitajika kuingia kwenye maombi mbele za Mungu kumuomba alisimamishe kusudi lake kwenye lango lako la uumbaji ili kupitia hilo kusudi la Mungu linaposimama kwenye hilo lango litadhihilisha maisha yako uliyokusudiwa na kupangiwa na Mungu kuyaishi. Shetani na nguvu za giza wakitaka usiweze kuishi maisha yako ya kusudi wanakubana na kupambana nawe katika lango la uumbaji ndio unatakiwa kuliombea sana mbele za Mungu hilo lango la uumbaji la kwako na watoto wako na wazazi wako na ndugu zako.
HATUA YA NNE YA KUOMBA:
( 4 ) Muombe Mungu akurejeshe katika Nafasi yako ya maisha sawasawa na nia yake ya kukuumba.
Waefeso 1:4 Mwanzo 3:9 Zaburi 118:5
🔵 Kila mtu kabla hajaubwa na Mungu kuna nafasi ya maisha ambayo Mungu alimkusudia hapa duniani na nafasi hiyo ipo kwenye ulimwengu wa roho, hivyo unatakiwa kwenda mbele za Mungu kumuomba akurejeshe katika nafasi yako ya maisha sawasawa na Nia yake ya kukuumba. Watu wengi kimaisha rohoni wameshatolewa kwenye nafasi zao ndio maana kwenye ulimwengu wa mwili mambo hayaendi kama yalivyotakiwa.
Hakikisha unapambana sana rohoni katika lango lako la uumbaji na kila roho zinazopambana nawe kimaisha. Kumbuka damu ya Yesu Kristo ina nguvu ya kukurejesha kwenye nafasi yako ya maisha itumie kwenye maombi yako haya unayoyapeleka mbele za Mungu Baba aloyekuumba na kukuleta hapa duniani.
HATUA YA TANO YA KUOMBA:
( 5 ) Hakikisha kwamba unaachilia Damu ya Yesu Kristo kila siku katika lango lako la Uumbaji.
Kutoka 12:23 Waebrania 12:24 Luka 22:20 Waebrania 9:19-22
Katika maombi yako ya kuombea lango la uumbaji la maisha yako hakikisha kwamba unaitumia damu ya Yesu Kristo kwenye hayo maombi yako katika hilo lango kwasababu ndani ya damu ya Yesu imebeba kazi nyingi sana hivyo unapoiachilia kwenye lango lako la uumbaji au lango la uumbaji la wazazi wako au watoto wako au ndugu zako hiyo damu ya Yesu Kristo itafanya kazi nyingi sana ikiwepo kutakasa hilo lango, kufungua hilo lango, kukomboa hilo lango n.k
Kama umeokoka wewe ni kuhani mbele za Mungu hivyo unaruhusiwa kuitumia damu ya Yesu Kristo, kaa kwenye maombi ya kuombea malango yako ya kiroho ukitumia damu ya Yesu Kristo na Jina la Yesu Kristo.
🔶 Nimekupatia hizo hatua 5 za kuombea lango lako la uumbaji mbele za Mungu hakikisha unakaa sana kwenye maombi na kuomba na Mungu yuko tayari kusikia na kujibu maombi yako. Baada ya kumaliza lango hili la uumbaji katika semina yetu ya kesho tutaingia lango lingine ambalo nataka tulishughulikie rohoni kwa maombi.
✔️ Kwa leo semina yetu inaishia hapa tukutane siku ya kesho hakikisha unatafakari somo la leo na kulitendea kazi kwa maombi. Nakuomba unisaidie kuwashirikisha watu wengine masomo haya ili nao wapate maarifa haya ya Neno la Mungu na kutoka kwenye mateso walionayo kimaisha.
Kwa mawasiliano nami utanipata kwa namba hizi, pia tumia hizi namba kumshukuru Mungu kwa Sadaka zako kupitia Semina hii kwenye madhabahu hii ya utumishi wake.
Vodacom M-PESA +255 765 867574.
Airtel Money +255 785 855785.
Tigo Pesa +255 673 784197.
Email address ni Pastorkibiriti@gmail.com
Mimi ni Mwalimu wa Neno la Mungu la Maarifa
Samwel Kibiriti.
Mei 29, 2021
@Kibiriti2021
Yesu Kristo anarudi kulichukua kanisa lake hakikisha kwamba umeokoka na kuishi maisha ya kupendezesha moyo wa Mungu kila siku.
No comments:
Post a Comment