Semina ya Siku 30 ( Christ For All People Church- Mbeya ).
KUYASHUGHULIKIA MALANGO YA KIROHO YANAYOGUSA MFUMO WAKO WA MAISHA YA KILA SIKU.
Day 3 ya Semina.
Na Mwalimu Samwel Kibiriti.
Asifiwe Yesu Kristo karibu mwana wa Mungu katika semina ya siku ya leo tena.
MFUMO WAKO WA MAISHA YA KILA SIKU UNAGUSWA NA MAMBO YAFUATAYO ( B ):
Tunaendelea pale tulipoishia katika semina ya jana ambapo nilikuonyesha mambo 7 yanayogusa mfumo wako wa maisha ya kila siku. Nataka utambue wazi kwamba ili uwe na maisha mazuri yale Mungu aliyokupangia na kukusudia wakati wa kukuumba ni lazima sana uombee haya maeneo ninayokufundisha kiroho kwasababu yanahusika kila siku kuugusa mfumo wako wa maisha uwe unajua au hujui, ndio maana nikiwa mwalimu wa Neno la Mungu nakufunulia siri hizi na kukupatia maarifa haya ninachotamani Mungu ayageuze maisha yako na uishi katika maisha yako halisi hapa duniani.
( 8 ) Mfumo wangu wa maisha unaguswa na nchi ninayoishi.
Mwanzo 12:1-3 Mathayo 12:40 ( Kutoka 12:12; 1:13-14 )
🔶 Nchi unayoishi inayagusa maisha yako ya kila siku kutokana na utendaji kazi wa kiroho wa mazingira ya nchi yenu, nataka ujue kwamba Mungu alimtenga Ibrahimu na nchi yake na kumpeleka nchi nyingine kwasababu kwenye ulimwengu wa kiroho mazingira ya nchi aliyokuwa anaishi Ibrahimu yalishikiliwa na roho za miungu. Ndivyo ilivyo mazingira mengi ya kiroho ya nchi nyingi duniani hayako chini ya utawala wa Mungu katika Yesu Kristo bali yako chini ya miungu na hivyo watu wengi maisha yao yamefungwa kupitia nchi wanazoishi kiroho.
❌Je unajua nchi unayoishi kiroho inafanyaje kazi? Hakikisha unaombea sana nchi unayoishi kila siku mbele za Mungu na kuyafungua maisha yako kutoke kwenye mazingira ya kiroho ya nchi yaliyotumika kuyafunga na kuyakwamisha maisha yako hapa duniani.
( 9 ) Mfumo wangu wa maisha unaguswa na Nyumba ninayoishi.
Amosi 3:11-12 Isaya 13:21-22 Kutoka 20:2 Luka 11:20-22
🔶 Nyumba unayoishi inahusika sana kiroho kila siku kugusa mfumo wako wa maisha na wako watu ambao maisha yao yamefungwa kwenye nyumba wanazoishi au walizowahi kuishi na kwasababu wanadamu wengi wanaamiji kwamba jambo la nyumba nila kimwili shetani na miungu wamefanikiwa kuyafunga maisha yao. Wako watu ambao Mungu husema nao kwenye ndoto kwamba wamefungwa ndani ya nyumba lakini hawaelewi, nisikilize kuota ndoto uko kwenye nyumba za zamani sana au kwenye nyumba uliyowahi kuishi huko nyuma au kutoa ndoto umefungiwa ndani ya nyumba ni ishara za kiroho kwamba nafsi yako imefungwa katika nyumba na huwezi ukafanikiwa kimaisha hadi ufanye maombi ya kujifungua katika hizo nyumba kiroho.
❌Je unajua utendaji kazi wa kiroho wa nyumba unayoishi? Je nyumba unayoishi iko chini ya utawala wa ufalme wa nani? Wewe fikiria unaishi kwenye nyumba ambayo iko chini ya utawala wa ufalme wa shetani/miungu unafikiri maisha yako au maisha yenu yatakuwaje? Lazima kujikuta unaishi kwenye maisha ya umasikini na kutokufanikiwa hata kama unajitahidi kufanya sana kazi, hakikisha unafanya maombi ya nguvu ya kufungua maisha yako na maisha yenu yaliyofungwa kwenye nyumba.
✔️ Kama unahitaji kupata maarifa mengi ya Neno la Mungu kuhusu Nyumba unayoishi nakuomba tafuta kitabu changu nilichoandika kiitwacho PATA MAARIFA YA KIROHO KUHUSU NYUMBA UNAYOISHI. Ndani ya kitabu nimefunua siri nyingi sana kuhusu nyumba na kuweka maombi mengi yatakayofungua maisha yako yaliyofungwa kwenye nyumba, kitabu ni Tsh 8,000 ( Elfu Nane ) tuwasiliane kwa maelezo zaidi.
( 10 ) Mfumo wangu wa maisha unaguswa na utendaji kazi wa Nafsi yangu.
Ayubu 33:18 Zaburi 25:13 Mithali 23:14 Isaya 38:15
🔶 Utendaji kazi wa nafsi yako ndio ulioamua aina ya maisha unayoyaishi sasa hivi, kwasababu nafsi ndio Injini ya maisha ya mwanadamu hivyo Nafsi yako kama imefungwa maana yake maisha yako yamefungwa hata kama hutaki pia kama Nafsi yako imetekwa ujue kwamba maisha yako yemshatekwa na yanaongozwa na mtu mwingine. Kuna watu mnajitahidi sana kufanya kazi na kusoma lakini hamfanikiwi na kufikia viwango vya juu kwasababu kiroho Nafsi zenu zimeshafungwa na kuharibikwa.
❌Je wewe unaujua utendaji kazi wa Nafsi yako kila siku kiroho? Watu wengi hamfanyi tathimini za Nafsi zenu hivyo kujikuta mnaishi tu kiholela ni lazima ufanye sana maombi ya kuifungua na kuikomboa nafsi yako ili iweze kurudi katika utendaji kazi uliokusudiwa na Mungu wakati wa kukuumba na hapo ndipo utayaona na maisha yako pia yakibadilika na kuwa kama vile Mungu alivyokukusudia.
( 11 ) Mfumo wangu wa maisha unaguswa na Madhabahu za kiroho.
Waamuzi 6:11-32 Kutoka 17:14-16
🔶 Madhabahu zilizopo kwenye ulimwengu wa roho zinahusika sana kugusa mfumo wako wa maisha ya kila siku inategemea wewe maisha yako rohoni yameshikiliwa na madhabahu ya nani ya Mungu au miungu. Kwa asilimia kubwa sana ya wanadamu maisha yao kiroho yameshikiliwa na madhabahu za miungu ndio maana hizo madhabahu za miungu zimewatengenezea aina ya maisha magumu sana na kushindwa kutoka hapo miaka na miaka.
❌Je wewe maisha yako rohoni yameshikiliwa na madhabahu ya nani? Wengi maisha yao hayajashikiliwa na madhabahu ya Mungu bali miungu hivyo unayo kazi kubwa kama aliyoifanya Gideoni ya kuvunja hizo madhabahu zilizoshikilia maisha yako au maisha yenu rohoni kisha kuyaunganisha maisha yako na madhabahu ya Mungu katika Yesu Kristo.
( 12 ) Mfumo wangu wa maisha unaguswa na maagano ya kiroho.
Mwanzo 17:7 Kutoka 23:32 Luka 22:20 Waebrania 9:16-17
🔶 Maagano ya kiroho yamehusika sana na yanazidi kuhusika sana kugusa mfumo wa maisha ya mwanadamu na maagano mengi yanayohusiana na mwanadamu sio maagano ya Mungu bali ya miungu kwa hawa watu kutokea kwenye familia zao na uzao wao na miji yao na nchi zao, hivyo maagano watu wanaokuzunguka wanayoyafanya na miungu migeni yanakuathiri sana kiroho katika maisha yako kama hutajua jinsi ya kuomba na kujiunganisha na agano la Damu ya Yesu Kristo. Wengi maisha yenu yamefungwa kwenye maagano ya miungu rohoni ndio maana mnaishi chini ya ndoto zenu za maisha na kupitia vipindi vigumu sana kimaisha unalo jukumu la kufanya maombi ya nguvu sana.
❌Je wewe kwenye ulimwengu wa roho umeruhusu maagano yapi yahusike na maisha yako? Hakikisha unavunja maagano yote ya miungu yaliyotumika kuyafunga maisha yako kisha uyaunganishe maisha yako kwenye agano la Mungu kupitia damu ya Yesu Kristo.
✔️ Kwa leo semina yetu inaishia hapa tukutane siku ya kesho ya 4 ya Semina ambapo nitakupatia maarifa mengine kuhusu malango ya kiroho. Nakuomba fanyia kazi kwa maombi somo hili la leo.
Kwa mawasiliano nami utanipata kwa namba hizi:
Vodacom +255 765 867574 ( WhatsApp ).
Airtel +255 785 855785.
Tigo +255 673 784197.
Kwa Email address ni Pastorkibiriti@gmail.com
Mimi ni Mwalimu wa Neno la Mungu la Maarifa
Samwel Kibiriti.
Mei 17, 2021
Mbeya Tanzania.
@Kibiriti2021
Naomba washirikishe watu wengine somo hili nao wapokee Maarifa haya ya Neno la Mungu ili maisha yao yafunguliwe na Yesu Kristo.