Huduma ya SISI NI KIZAZI CHA KUSUDI LA MUNGU HAPA DUNIANI inakuletea kipindi cha Tafakari ya Neno la Mungu.
TAFAKARI YA KITABU CHA KUTOKA SURA YA 19:5-6 KUWA TUNU MBELE ZA MUNGU.
Bwana Yesu Kristo asifiwe mwana wa Mungu na Rafiki yangu naomba Leo tuweze kutafakari mistari hii ili kupata Maarifa na Ufahamu wa Neno la Mungu maishani mwetu.
KUTOKA 19:5-6 inasema kuwa
"Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu, nanyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani, na taifa takatifu. Hayo ndiyo maneno utakayowaambia wana wa Israeli".
Tafsiri ya Neno Biblia inasema
"Sasa kama mkinitii kikamilifu na kutunza Agano langu, basi ninyi mtakuwa mali yangu ya thamani kubwa miongoni mwa mataifa yote. Ijapokuwa dunia yote ni mali yangu, ninyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani na taifa takatifu.’ Haya ndiyo maneno utakayosema kwa wana wa Israeli".
Tafsiri ya Biblia ya Katiba ya Ufalme inasema
"Sasa kama mkinitii kikamilifu na kutunza agano langu, basi ninyi mtakuwa mali yangu ya thamani kubwa miongoni mwa mataifa yote. Ijapokuwa dunia yote ni mali yangu, ninyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani na taifa takatifu.’ Haya ndiyo maneno utakayosema kwa wana wa Israeli".
🔶 Katika mistari hii yote ambayo nimekuonyesha katika tafsiri hizi 3 za Biblia Kuna mambo ambayo nataka uyaone hapa yaliyoahidiwa kwetu na Mungu Baba kwa sisi kuwa TUNU kwake na neno hili TUNU maana yake ni kuwa Mali yake Mungu ya thamani.
JAMBO LA KWANZA:
Mungu Baba ameahidi wazi kwamba ili tuwe TUNU kwake ni lazima TUITII KIKAMILIFU SAUTI YAKE.
🟡 Tunapokubali kila siku kuishi maisha ya kuitii SAUTI ya Mungu na kuyafanyia kazi Yale yote yaliyomo Ndani ya SAUTI ya Mungu hapo sisi tutakuwa TUNU mbele za Mungu na kuwa tofauti na wanadamu wengine kwasababu tutakuwa wa thamani machoni pa Mungu. Maisha yetu yameshindwa kuleta matokeo makubwa hapa duniani kama watoto wa Mungu kwasababu tumekuwa sio watii wa sauti ya Mungu mara nyingi tumekuwa watu wa kupuuzia na kudharau SAUTI ya Mungu inayopatikana katika Neno lake na inayopatikana kwa Roho Mtakatifu.
Hivyo nakuomba mwana wa Mungu kama unahitaji uishi maisha yaliyojaa utukufu wa Mungu hapa duniani ambayo yatakutenganisha na wanadamu wengine ni lazima ukubali sasa hivi kuishi katika maisha ya kuitii KIKAMILIFU SAUTI ya Mungu pasipo kujali watu watakuelewaje ila itii SAUTI ya Mungu na kufanya yote yanayotoka katika SAUTI ya Mungu hata kama nafsi yako itapiga kelele Kubali kuitii SAUTI ya Mungu kila siku nawe utakuwa TUNU mbele za Mungu.
JAMBO LA PILI:
Mungu Baba ameahidi wazi kwamba ili tuwe TUNU kwake ni lazima TULITUNZE AGANO LAKE.
🟣 Hatutaweza kuwa TUNU mbele za Mungu kama hatutaweza kulitunza Agano lake nataka Ufahamu kuwa Mungu ametuumba Ndani ya Agano lake la Ufalme kwasababu tunayo sura na mfano wake hii ni ishara ya kiroho kwamba tumeumbwa na Mungu katika Agano la Ufalme wake na alipotuleta hapa duniani ametupa Katiba yake ambayo ni Neno lake na Neno la Mungu limebeba Agano kati ya Mungu na mwanadamu hivyo tunatakiwa kila siku ya maisha yetu hapa duniani tuishi sawasawa na misingi yote ya Neno la Mungu inavyotuelekeza na kusema.
Sababu ya maisha yetu kutokuwa ya thamani kubwa hapa duniani na kujikuta tunadharauliwa sana na maadui ni kwasababu sisi wenyewe tumekataa kulitunza Agano la Mungu ambalo ni Neno lake, Ndani ya Neno la Mungu tokea kitabu cha mwanzo hadi Ufunuo wa Yohana kimebeba maagizo na maelekezo ya Mungu juu yetu vile tunavyotakiwa kuishi kila siku katika mwenendo na tabia na usemi na matendo pia Neno la Mungu limebeba mwongozo kwamba tunatakiwa kuishi maisha ya kumwabudu na kumtumikia Mungu na kufanya mapenzi yake na kulitumikia Kusudi lake na kumwakilisha yeye katika kila eneo la maisha yetu lakini tulio wengi hatuishi sawasawa na Agano la Neno la Mungu linavyotutaka bali tunaishi tunavyotaka au tunavyoamua.
Hivyo Leo nakuomba ukubali kufanya maamuzi toka moyoni mwako kurejea kwa Mungu kwa kulitunza Agano lake ambalo ni Neno lake Kubali kuishi katika Msingi wa Neno la Mungu kila siku na kila wiki na kila mwezi na kila mwaka utakapokubali kuishi Katika Msingi wa Neno la Mungu wewe mbele za Mungu utakuwa TUNU kwake kuliko makabila yote na maisha yako yataang'aza kila siku na kila mahali utakapokuwa utakuwa Nuru ya Ufalme wa Mungu na utaishi maisha ya Baraka na mafanikio na ushindi.
JAMBO LA TATU:
Mungu Baba ameahidi wazi kwamba kwa kuwa sisi ni TUNU kwake basi sisi ni UFALME WA MAKUHANI NA TAIFA TAKATIFU kwake.
🟢 Unatakiwa ujione kwa muonekano wa Neno la Mungu linavyosema sio ujione kwa muonekano wa wanadamu wanavyosema au shetani na maadui wanavyosema hapa Mungu wetu anasema wazi kwamba kwasababu tumekuwa TUNU kwake sisi ni UFALME WA MAKUHANI na TAIFA TAKATIFU sio sio washenzi na mambumbumbu au sisi sio wajinga na wapumbavu au sisi sio wagonjwa na maskini na mafukara n.k
Kuna makosa makubwa sana ambayo ninayaona kwa Wakristo wengi walio wana wa Mungu wanajitafsiri na kujiona kama wanadamu wengine wanavyowasema au kama maadui na watesi wao wanavyowasema au kama shetani na miungu inavyowasema au kama viongozi wao wa siasa wanavyowasema na maneno hayo wameyatunza na kuyakumbatia mioyoni mwao kumbe walichokishika na kukikumbatia mioyoni mwao ni uongo tu wa shetani kupitia hayo maneno
Nataka nikuambie mwana wa Mungu na Rafiki yangu ni kwamba ukweli wa tafsiri original ya maisha yako ni Neno la Mungu vile Mungu amesema na vile Yesu Kristo amesema na vile Roho Mtakatifu anasema kuhusu wewe huo ndio ukweli unaotakiwa kuukumbatia moyoni mwako na kuishi nao. Kuanzia SASA hivi ishi katika fikra hii na mawazo haya na ukiri huu kwamba
"Mimi..... Ninakiri wazi mbele zako Mungu Baba sawasawa na Neno lako ambalo umesema nami muda huu katika kitabu cha Kutoka 19:5-6 Mimi ni TUNU ya Ufalme wako kuliko makabila yote na Mimi ni Ufalme wa makuhani kwako Mungu na taifa takatifu, Asante kwa Baraka zako za ukuhani na Ufalme juu ya maisha yangu na hapa duniani nitafanikiwa katika kila jambo ninalofanya nami nitastawi na kuzaa na kuongezeka na kutawala na kumiliki kwaajili ya Kusudi lako Mungu Baba na ulinzi wako na uwepo wako na Kibali chako kipo juu ya maisha yangu kwa Jina la Yesu Kristo ninaomba na kushukuru maana nimeamini umetenda kwangu rohoni na mwilini Amen".
KAMA BADO HUJAOKOKA OMBA SALA HII KWA IMANI TOKA MOYONI MWAKO ILI UFANYIKE MTOTO WA MUNGU.
Mungu nakushukuru kwa upendo wako juu ya maisha yangu umeniumba na kunileta hapa duniani kwaajili ya Kusudi la Ufalme wako lakini kwa miaka mingi nimeishi maisha ya dhambi na uovu lakini Leo toka Ndani ya moyo wangu ninajutia maisha niliyoyaishi ya chukizo kwako nami nimeufungua moyo wangu na kumruhusu Yesu Kristo awe Bwana na mwokozi wa maisha yangu kwasababu alikufa na kufufuka kwaajili yangu, ninaomba Bwana Yesu ulifute jina langu katika kitabu cha hukumu na kuliandika upya katika kitabu cha uzima nami Leo nimekuwa kiumbe KIPYA na maisha yangu yameungana nawe Bwana Yesu nitaishi maisha ya kuzaa matunda kwaajili ya Ufalme wa Mungu kila siku hapa duniani katika Jina la Yesu Kristo ninakiri waziwazi kwamba mimi nimeokoka Amen.
✅ Hongera sana kwa maamuzi haya muhimu ambayo umefanya leo na sasa wewe ni mwana wa Mungu karibu katika Ufalme wa Mungu na Roho Mtakatifu atakuwa kiongozi wa maisha yako kila siku, nategemea kupata taarifa njema kwamba Mtumishi Mimi katika Ibada hii nimeokoka tumia number hii ya Huduma +255 765 867574 ili nizidi kukuombea mbele za Mungu udumu katika maisha haya mapya ya wokovu.
Mimi ni rafiki yako katika Kristo Yesu
Mwalimu Samwel Kibiriti.
➡️ Nikukaribishe kupokea BARAKA ZA MUNGU KWA NJIA YA UTOAJI SADAKA YAKO KATIKA MADHABAHU HII YA UTUMISHI ambapo unaweza kutumia number hii ya Huduma +255 765 867574 na Sadaka zako zitafika Madhabahuni pa Mungu na kutumika katika Kuujenga Ufalme wake.
Songea, Ruvuma Tanzania.
Karibu tena katika mfululizo wa masomo haya ya Tafakari siku ya kesho tena washirikishe na wengine.
NAOMBA UWEZE KUANDIKA KWENYE COMENT KILE AMBACHO UMEJIFUNZA KATIKA SOMO LA TAFAKARI YA LEO, KARIBU.
No comments:
Post a Comment