Post Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 29, 2017

3:35 AM

MAOMBI YA KUMKUMBUSHA MUNGU.

AINA TOFAUTI ZA MAOMBI.


Shalom karibu tena tuendelee kujifunza somo hili la aina tofauti za maombi.



{ KIPENGELE CHA TISA }.

Kuna Maombi ya Kumkumbusha Mungu.

Haya ni maombi pia ambayo unatakiwa umuombe Mungu yaani ni mfumo wa kumuomba Mungu kwa kumkumbusha kwa yale aliyokuahidi kwamba atakutendea kwenye maisha yako lakini amekawia kukupatia.

  Inawezekana kabisa ni kweli Mungu amekuahidi ahadi nyingi kwamba atakutendea kwenye maisha yako lakini bado hizo ahadi hazijadhihilika katika maisha yako, kwahiyo unachotakiwa ni kumwendea Mungu kwa mfumo huu wa maombi ya kumkumbusha kwamba Mungu uliniahidi kwamba utanitendea jambo Fulani lakini bado hujanitendea leo nakuja mbele zako kukukumbusha Baba ili unitimilizie jambo hilo kwenye maisha yangu.

                               Isaya 43

26 Unikumbushe; na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako.

   Mungu anasema tumkumbushe, sasa anaposema kwamba tumkumbushe haina maana kwamba amesahau Mungu hapana ila anachotaka ni kuona kwamba unaouhitaji ndani ya moyo wako wa kumuona Mungu anatimiza zile ahadi alizokueleza/kukuahidia kwahiyo unapomkumbusha Mungu maana yake anaona kwamba kumbe ndani ya moyo wako unamtaka yeye akitimizie hizo ahadi kwenye maisha yako.

    Nitahitaji usome kitabu cha MALAKI 3:13-18 utaona watu waliokuwa wanamtumikia Mungu wanasemezana maneno magumu sana mbele za Mungu kwamba hakuna faida ya kumtumikia Mungu ndipo akawajibu na kuwaambia kwamba “Ndipo wale waliomcha BWANA waliposemezana wao kwa wao. Naye BWANA akasikiliza, akasikia; na kitabu cha Ukumbusho kikaandikwa mbele zake, kwa ajili ya hao waliomcha BWANA, na kulitafakari jina lake”.

Unaona kule mbinguni Mungu anacho kitabu cha Ukumbusho kwahiyo unapomuomba Mungu maombi haya ya kumkumbusha maana yake unamuomba Mungu arudi kwenye hicho kitabu chake cha ukumbusho na aangalie zile ahadi alizokuahidia kwamba atakutendea kwenye maisha yako.

  Ukisoma pia kwenye kitabu cha Isaya 38:1-6 wakati Hezekia alipokuwa mgonjwa na kupewa taarifa kwamba atakufa aligeuka ukutani na kumkumbusha Mungu na Mungu akamsikia na kukumbuka mambo aliyowahi kuyatenda huko nyumba kwenye ufalme wake.


     Ndio maana kuna kipindi cha maisha kinafika unachotakiwa ni kuingia kwenye maombi haya ya kumkumbusha Mungu kwamba Mungu kumbuka mambo niliyofanya kwenye ufalme wako na Mungu ataenda kwenye kitabu hicho cha ukumbusho na kuangalia utumishi wako naye atakujibu na kukutendea au kukuvusha mahali pagumu sana kimaisha.

   Mungu akubariki sana tukutane tena siku ya kesho.

kwa mawasiliano nami utanipa kwa simu hizi:

vodacom +255 765 867574.

tigo          +255 673 784197.

Airtel       +255 785 855785.

Kwa Email ni  Pastorkibiriti@gmail.com

July 29, 2017.


                     Mwalimu Samwel Kibiriti.


Friday, July 28, 2017

12:56 AM
LEO IJUMAA TAREHE 28/07/2017 SEMINA YETU INAINGIA SIKU YA TANO HAPA BOMA HAI KILIMANJARO.

KARIBU USHIRIKI NASI KATIKA SEMINA HII HAPA KATIKA HEMA YA HUDUMA YA FIRE FIRE UKOMBOZI KARIBU NA SHULE YA SEKONDARY SHELELA.

AU FUATANA NAMI KATIKA SEMINA HII KUPITIA UKURASA WANGU WA FACEBOOK AMBAO NI Samwel Kibiritiministry

UBARIKIWE SANA NA IJUMAA NJEMA SANA KWAKO.
12:48 AM

MAOMBI YA ULINZI.

AINA TOFAUTI ZA MAOMBI.

Bwana Yesu Kristo asifiwe sana.

karibu tena ndani ya blog hii uweze kupokea maarifa haya ya kiroho.




{ KIPENGELE CHA NANE }

Kuna Maombi ya Ulinzi.

Haya ni maombi ambayo unatakiwa sana kumuomba Mungu kwa sababu katika dunia hii tunayoiishi tumezungukwa na adui yetu mkuu shetani pamoja na wajumbe/ vibaraka vyake ambao ni wachawi, waganga wa kienyeji, mapepo, majini, mizimu, maadui n.k 

    kwahiyo ni lazima umuombe Mungu kila siku ili akulinde na kulinda familia yako/yenu, kuwalinda watoto wako, kulinda mali zako n.k

                        AYUBU 1

9 Ndipo Shetani akamjibu BWANA, na kusema, je! Huyo Ayubu yuamcha BWANA bure?

10 Wewe hukumzingira kwa ukigo/ukuta pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo? Kazi za mikono yake umezibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika nchi.

Hapa unayakuta ni mazungumzo kati ya Mungu na Shetani wakati Shetani ametokea huku duniani Mungu akamuuliza Shetani kwamba je amemuona huyo mtumishi wake Ayubu, na Shetani akamjibu Mungu kwamba amemzunguzia ulinzi Ayubu kwahiyo kutokana na ule ulinzi kwa Ayubu na nyumba yake na mali zake ulimfanya asiweze kumshambulia na kumpiga Ayubu.

  Kwahiyo sasa unamuona Shetani anamshawishi Mungu auondoe ule ulinzi wake kwa Ayubu na nyumba yake na mali zake ili aweze kumshambulia na kumpiga, ndio maana Mungu alipomuondolea Ayubu ule ulinzi wake akapata nafasi ya kumpiga na kumshambulia.

   Kwahiyo sasa unatakiwa sana umuombe Mungu ulinzi wake katika maeneo yote ya maisha yako yaani muombe Mungu akulinde wewe mwenyewe, alinde mali zako, alinde watoto wako, alinde wazazi wako, alinde nyumba yako, ayalinde masomo yako n.k ili shetani na wachawi na waganga wa kienyeji na mapepo na majini na roho za mizimu zisiweze kukushambulia.

   Hakikisha usiku na mchana unamuomba Mungu ulinzi wake kwenye kila eneo la maisha yako.

    Kwa mawasiliano nami utanipata kwa simu namba hizi:


Vodacom +255 765 867574.


Tigo         +255 673 784197.


Airtel       +255 785 855785.


kwa Email utanipata kwa   Pastorkibiriti@gmail.com


blogsport: Samwel Kibiritiministry.blogsport.com


July 28, 2017.


Mwalimu Samwel Kibiriti.




                                

Thursday, July 27, 2017

6:51 AM

SEMINA YA NENO LA MUNGU.

KARIBU SANA KATIKA SEMINA HAPA BOMA, HAI, KILIMANJARO.



Bwana Yesu asifiwe sana mwana wa Mungu,

ninayo semina ya siku nane { 8 } hapa katika mji wa bomang'ombe, wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro, katika nchi ya Tanzania, kuanzia tarehe 23 hadi 30/07/2017.

Semina hii ninairusha moja kwa moja Live kila siku kuanzia saa 11 jioni katika ukurasa wangu wa Facebook ambao ni   "Samwel Kibiritiministry".

Ungana nasi kwa njia ya maombi yako kuombea semina hii.

Somo la Semina ambalo Mungu alinipatia linakichwa kinachosema  "KWANINI MTU ALIYEOKOKA ANAHITAJI KUFUNGULIWA?". hili ni somo la msingi sana kwa kila mtu aliyeokoka kulifahamu.

Mungu Baba ayahifadhi maisha yako naya uzao wako milele.

                        Mwalimu wa Semina 
                             Samwel Kibiriti.

Featured Post

JINSI MISINGI YA VIZAZI INAVYOWEZA KUKAMATA MAISHA YAKO.

Fahamu kwamba misingi ni chanzo au asili au chimbuko la mtu. Na msingi wako wa vizazi unatokana na ukoo wako na kabila lako.      ...