AINA TOFAUTI ZA MAOMBI.
Bwana Yesu Kristo asifiwe sana.
karibu tena ndani ya blog hii uweze kupokea maarifa haya ya kiroho.
{ KIPENGELE CHA NANE }
Kuna Maombi ya Ulinzi.
Haya ni maombi ambayo unatakiwa sana
kumuomba Mungu kwa sababu katika dunia hii tunayoiishi tumezungukwa na adui
yetu mkuu shetani pamoja na wajumbe/ vibaraka vyake ambao ni wachawi, waganga
wa kienyeji, mapepo, majini, mizimu, maadui n.k
kwahiyo ni lazima umuombe Mungu
kila siku ili akulinde na kulinda familia yako/yenu, kuwalinda watoto wako,
kulinda mali zako n.k
AYUBU 1
9 Ndipo Shetani akamjibu BWANA, na
kusema, je! Huyo Ayubu yuamcha BWANA bure?
10 Wewe hukumzingira kwa ukigo/ukuta
pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo? Kazi za mikono
yake umezibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika nchi.
Hapa unayakuta ni mazungumzo kati ya
Mungu na Shetani wakati Shetani ametokea huku duniani Mungu akamuuliza Shetani
kwamba je amemuona huyo mtumishi wake Ayubu, na Shetani akamjibu Mungu kwamba amemzunguzia
ulinzi Ayubu kwahiyo kutokana na ule ulinzi kwa Ayubu na nyumba yake na mali
zake ulimfanya asiweze kumshambulia na kumpiga Ayubu.
Kwahiyo sasa unamuona Shetani anamshawishi Mungu auondoe ule ulinzi wake
kwa Ayubu na nyumba yake na mali zake ili aweze kumshambulia na kumpiga, ndio
maana Mungu alipomuondolea Ayubu ule ulinzi wake akapata nafasi ya kumpiga na
kumshambulia.
Kwahiyo sasa unatakiwa sana umuombe
Mungu ulinzi wake katika maeneo yote ya maisha yako yaani muombe Mungu akulinde
wewe mwenyewe, alinde mali zako, alinde watoto wako, alinde wazazi wako, alinde
nyumba yako, ayalinde masomo yako n.k ili shetani na wachawi na waganga wa
kienyeji na mapepo na majini na roho za mizimu zisiweze kukushambulia.
Kwa mawasiliano nami utanipata kwa simu namba hizi:
Vodacom +255 765 867574.
Tigo +255 673 784197.
Airtel +255 785 855785.
kwa Email utanipata kwa Pastorkibiriti@gmail.com
blogsport: Samwel Kibiritiministry.blogsport.com
July 28, 2017.
Mwalimu Samwel Kibiriti.
Amen
ReplyDeleteAsante kwa mafundisho mazuri
ReplyDeleteAmen.
ReplyDelete