AINA TOFAUTI ZA MAOMBI.
Shalom karibu tena tuendelee kujifunza somo hili la aina tofauti za maombi.
{ KIPENGELE CHA TISA }.
Kuna Maombi ya Kumkumbusha Mungu.
Haya ni maombi pia ambayo unatakiwa
umuombe Mungu yaani ni mfumo wa kumuomba Mungu kwa kumkumbusha kwa yale
aliyokuahidi kwamba atakutendea kwenye maisha yako lakini amekawia kukupatia.
Inawezekana kabisa ni kweli Mungu amekuahidi ahadi nyingi kwamba
atakutendea kwenye maisha yako lakini bado hizo ahadi hazijadhihilika katika
maisha yako, kwahiyo unachotakiwa ni kumwendea Mungu kwa mfumo huu wa maombi ya
kumkumbusha kwamba Mungu uliniahidi kwamba utanitendea jambo Fulani lakini bado
hujanitendea leo nakuja mbele zako kukukumbusha Baba ili unitimilizie jambo
hilo kwenye maisha yangu.
Isaya 43
26 Unikumbushe; na tuhojiane; eleza
mambo yako, upate kupewa haki yako.
Mungu anasema tumkumbushe, sasa
anaposema kwamba tumkumbushe haina maana kwamba amesahau Mungu hapana ila
anachotaka ni kuona kwamba unaouhitaji ndani ya moyo wako wa kumuona Mungu anatimiza
zile ahadi alizokueleza/kukuahidia kwahiyo unapomkumbusha Mungu maana yake
anaona kwamba kumbe ndani ya moyo wako unamtaka yeye akitimizie hizo ahadi
kwenye maisha yako.
Nitahitaji usome kitabu cha MALAKI 3:13-18 utaona watu waliokuwa
wanamtumikia Mungu wanasemezana maneno magumu sana mbele za Mungu kwamba hakuna
faida ya kumtumikia Mungu ndipo akawajibu na kuwaambia kwamba “Ndipo
wale waliomcha BWANA waliposemezana wao kwa wao. Naye BWANA akasikiliza,
akasikia; na kitabu cha Ukumbusho kikaandikwa mbele zake, kwa ajili ya hao
waliomcha BWANA, na kulitafakari jina lake”.
Unaona kule mbinguni Mungu anacho
kitabu cha Ukumbusho kwahiyo unapomuomba Mungu maombi haya ya kumkumbusha maana
yake unamuomba Mungu arudi kwenye hicho kitabu chake cha ukumbusho na aangalie
zile ahadi alizokuahidia kwamba atakutendea kwenye maisha yako.
Ukisoma pia kwenye kitabu cha Isaya 38:1-6 wakati Hezekia alipokuwa
mgonjwa na kupewa taarifa kwamba atakufa aligeuka ukutani na kumkumbusha Mungu
na Mungu akamsikia na kukumbuka mambo aliyowahi kuyatenda huko nyumba kwenye
ufalme wake.
Ndio maana kuna kipindi cha maisha kinafika unachotakiwa ni kuingia
kwenye maombi haya ya kumkumbusha Mungu kwamba Mungu kumbuka mambo niliyofanya
kwenye ufalme wako na Mungu ataenda kwenye kitabu hicho cha ukumbusho na
kuangalia utumishi wako naye atakujibu na kukutendea au kukuvusha mahali pagumu
sana kimaisha.
Mungu akubariki sana tukutane tena siku ya kesho.
kwa mawasiliano nami utanipa kwa simu hizi:
vodacom +255 765 867574.
tigo +255 673 784197.
Airtel +255 785 855785.
Kwa Email ni Pastorkibiriti@gmail.com
July 29, 2017.
Mwalimu Samwel Kibiriti.
No comments:
Post a Comment