Post Top Ad

Post Top Ad

Thursday, July 29, 2021

 Semina ya siku 30 ( Christ For All People Church- Mbeya ).


KUYASHUGHULIKIA MALANGO YA KIROHO YANAYOGUSA MFUMO WAKO WA MAISHA YA KILA SIKU.


             Day 14 ya semina.


Senior Pastor Samwel Kibiriti.


Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu karibu tuendelee na semina ya siku ya leo.


KUSHUGHULIKIA LANGO LA UUMBAJI WAKO.


Mwanzo 1:26-27; 5:1-2


Naomba nikuingize ndani kidogo katika semina ya lango hili la uumbaji kiroho.


JINSI YA KUOMBEA LANGO LAKO LA UUMBAJI MBELE ZA MUNGU ( A ).


Katika semina ya siku ya leo na siku ya kesho nataka nikufundishe jinsi gani unaweza kuombea lango lako la uumbaji au malango ya uumbaji ya watoto wako au wazazi wako au ndugu zako mbele za Mungu kila siku. Kwasababu wengi wenu hamuombei lango la uumbaji wenu kutokana na kutokuwa na maarifa ya kiroho lakini kupitia semina hii inakupatia ufahamu utakaokaa nao mbele za Mungu kwa maombi yako.


HATUA YA KWANZA YA KUOMBA:


( 1 ) Omba toba kwa Mungu kwaajili ya maisha yako unayoishi hapa duniani.


1Yohana 1:8-10 Waefeso 4:27 Warumi 3:23


🟤 Unahitajika kuomba toba mbele za Mungu kwaajili ya maisha yako unayoishi hapa duniani kama unahitaji msaada wake Mungu kwenye lango lako la uumbaji pia kama unamuombea mtu mwingine kwenye lango lake la uumbaji hakikisha unaomba toba mbele za Mungu kwaajili yake. Kumbuka dhambi ndio iliyompatia shetani uhalali wa kushikilia lango lako la uumbaji au lango la uumbaji la huyo unayemuombea ndio maana lazima uanze na maombi ya toba mbele za Mungu.


HATUA YA PILI YA KUOMBA:


( 2 ) Vunja roho za asili ya kuzaliwa kwako ambazo zinatenda kazi katika lango lako la uumbaji.


Ezekieli 16:1-4 Yohana 10:36; 16:21 Mhubiri 4:14


🔴 Kati ya roho ambazo zimesababisha kuwazuia watu wasiweze kuishi maisha yao waliyopangiwa na Mungu wakati wa kuumbwa kwao ni roho za asili ya kuzaliwa kwao zimekuwa zikisimama kinyume na maisha ya watu wengi kiroho, hivyo unatakiwa kuingia kwenye maombi ya kuvunja roho za asili ya kuzaliwa kwako ambapo zinafanya kazi katika lango lako la uumbaji kiroho.


Historia za kuzaliwa kwa watu wengi sio nzuri kabisa kutokea kutungwa kwao mimba na miezi tisa waliyokaa tumboni mwa mama zao na kuzaliwa kwao na vitu walivyofanyiwa baada ya kuzaliwa kuna mazingira mengi ya kishirikina na kimila yamefanyika hivyo kutoa uhalali kwa roho mbalimbali za giza kupata nafasi ya kuwashikilia na kuwatawala na kuongoza maisha yao rohoni na hivyo kukuta katika ulimwengu wa mwili wanateseka na kuhangaika kimaisha kila siku na jambo hili haliufurahishi moyo wa Mungu.


🔶 Nakuomba fanya maombi ya nguvu ya kuvunja roho za asili ya kuzaliwa kwako ambazo zinafanya kazi kwenye lango lako la uumbaji pia vunja hizo roho za asili katika maisha ya watoto wako na wazazi wako na ndugu zako zinazofanya kazi katika lango lao la uumbaji. Hakikisha unayafungua maisha yako pia yaliyokuwa yamefungwa na roho za asili ya kuzaliwa kwako kwa jina la Yesu Kristo na matokeo makubwa utayaona kwenye maisha yako ya kila siku hapa duniani.


✔️ Kwa leo semina yetu inaishia hapa hakikisha unafanyia kazi kwa maombi somo hili mpaka siki ya kesho tutakapokutana ambapo nitakuonyesha hatua nyingine za kuombea lango lako la uumbaji mbele za Mungu. Naomba unisaidie kuwatumia wengine somo hili ili wapokee Ufahamu huu wa Neno la Mungu na wasiendelee kuishi kwa mateso katika maisha yao.


Kwa mawasiliano nami utanipata kwa namba hizi, pia unaweza kutumia hizi namba kumshukuru Mungu kwa Sadaka zako katika hii madhabahu ya utumishi wake.


Vodacom M-PESA +255 765 867574 ( WhatsApp ).


Airtel Money +255 785 855785


Tigo Pesa +255 673 784197


Kwa Email address ni Pastorkibiriti@gmail.com


Mimi ni Mwalimu wa Neno la Mungu la Maarifa



           Samwel Kibiriti.


Mei 28, 2021

@Kibiriti2021


Tukutane katika semina ya siku ya kesho hakikisha unamtumikia Mungu katika maisha yako kwa nguvu zako zote.

No comments:

Post a Comment

Featured Post

JINSI MISINGI YA VIZAZI INAVYOWEZA KUKAMATA MAISHA YAKO.

Fahamu kwamba misingi ni chanzo au asili au chimbuko la mtu. Na msingi wako wa vizazi unatokana na ukoo wako na kabila lako.      ...