AINA TOFAUTI ZA MAOMBI.
SOMO LA KWANZA 2017
Nakukaribisha sana ndani ya darasa hili la kupokea maarifa ya kiroho sawa sawa na vile ambavyo Roho Mtakatifu atatuongoza kujifunza
.
Naamini kwamba somo la kuomba au maombi umelisikia sana likifundishwa sana na watumishi wa Mungu maeneo mbalimbali.
Sasa Mimi katika SOMO hili limelenga mambo haya yafuatayo:
1 Kukuonyesha AINA tofauti tofauti za maombi.
2 Kutokana na wewe kuelewa hizi aina tofauti za maombi utabadilisha uelewa wako kuhusu maombi, kwa sababu inawezekana kuna makosa unayoyafanya kuhusu maombi.
3 Kupitia somo hili litakusaidia kupata majibu kutokana na kuomba kwako.
Kwahiyo fungua moyo wako ili Roho Mtakatifu aweze kusema nawe kupitia somo hili.
Na somo hili nitaligawa kwenye vipengele tofauti tofauti, kwahiyo hakikisha kwamba unafuatilia kipengele kimoja baada ya kingine. Karibu twende pamoja.
{ KIPENGELE CHA KWANZA }
KUNA MAOMBI YA KULALAMIKA.
Wako watu wengi sana ambao wanajua kwamba wanaomba kumbe wanalalamika lakini hawaombi Bali wanamlalamikia Mungu.
HABAKUKI 1
2 Ee BWANA, nilie hata lini, wewe usitake kusikia? Nakulilia kwa sababu ya udhalimu, ila hutaki kuokoa.
3 Mbona wanionyesha uovu, na kunitazamisha ukaidi? Maana uharibifu na udhalimu u mbele yangu; kuna ugomvi, na mashindano yatokea.
4 Kwa sababu hiyo sheria imelegea, wala hukumu haipatikani; kwa maana watu wabaya huwazunguka wenye haki; kwa sababu hiyo hukumu ikipatikana imepotoka.
➡ Hii ni habari ya Nabii Habakuki unamuona analalamika sana kuhusu mji aliokuwa anaishi yako mambo mabaya yalikuwa yanaendelea ndani ya huo mji.
Akajikuta badala ya kuomba na kumuomba Mungu akawa analalamika kutokana na mambo Yale aliyokuwa anayaona kwenye huo mji.
HABAKUKI 2
"1 Mimi nitasimama katika zamu yangu, nitajiweka juu ya mnara, nitaangalia ili nione atakaloniambia, na jinsi nitakavyojibu katika habari ya kulalamika kwangu".
Unamuona Nabii Habakuki akiweka wazi kwamba katika sura ya kwanza aliwekwa na Mungu katika zamu aombe kwaajili ya mji aliokuwamo lakini akawa analalamika badala ya kuomba, na Mungu alinyamaza kimya wakati analalamika hakumjibu.
Na katika hii sura ya pili ya Habakuki ndio unaona sasa akaamua kusimama katika zamu yake na Kumuomba Mungu na akaacha kulalamika.
✔ Nataka nikuulize swali hili wewe Rafiki yangu Je wewe katika maombi unamuomba Mungu au unamlalamikia Mungu?
Wengi sana hawaombi Bali wanalalamika.
➡ Sikiliza Mungu anaweza kukuonyesha mambo ya udhalimu na uovu kwenye hilo eneo unaloishi, kufanyia kazi, au hapo unaposali kama alivyomuonyesha Habakuki, Je Ukiyaona mambo hayo unamuomba Mungu aingilie kati na kuondoa huo udhalimu, uovu, ugomvi, na kupatikana kwa haki kwenye huo mji au unalalamika unapoyaona mambo hayo?
✔ Je hayo mambo mabaya unayoyaona ndani ya familia yako na ukoo wako unamuomba Mungu ayaondoe au unalalamika kutokana na kuona mambo hayo?
➡ Nakuomba badilisha mtazamo wako kuanzia sasa hivi kuhusu Maombi acha kulalamika Bali omba.
Acha kulalamika kwaajili ya mambo mabaya unayoyaona kwenye Nchi, serikali, kwenye familia yako/yenu, kwenye ukoo wenu, kwenye mji unaoishi na kufanyia kazi, kwenye shule unayosoma, kwenye kanisa/huduma, n.k
Acha kulalamika Bali ingia kwenye maombi na muombe Mungu abadilishe hayo unayoyaona na kuyasikia.
Tukutane siku ya kesho tukiangalia kipengele cha pili. Fanyia kazi kipengele hiki tulichojifunza.
Neema ya Kristo Yesu ikuongoze.
Kwa mawasiliano nami utanipata kwa namba hizi
Vodacom 0765 867574
Tigo 0673 784197
Airtel 0785 855785.
KAULI MBIU YA MWAKA 2017.
( 1 ) Acha dhambi.
( 2 ) Yesu Kristo anakuja.
( 3 ) Ishi katika maisha ya Utakatifu kila siku.
Mimi ni mwalimu Samwel Kibiriti Rafiki yako katika Kristo Yesu.
@2017, February 1
YOUR DESCRIPTION HERE
samwelkibiritiministry.blogspot.com|By Chuo Cha Maarifa ya Kiroho
No comments:
Post a Comment