Post Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 2, 2017

MUNGU HAPOKEI SADAKA YA MTU MWOVU.

        TAHADHARI JUU YA KANISA.



MIMI SITANYAMAZA KABISA NITAELEZA KWELI YA NENO LA MUNGU.

                            ISAYA 62:1

"Kwa ajili ya Sayuni ( Kanisa ) SITANYAMAZA, na kwa ajili ya Yerusalem sitatulia,....."

Siwezi kunyamaza kabisa kuona Neno la Mungu linapindishwa na Kanisa kutokuelezwa kweli ya Mungu. Pia siwezi kunyamaza kuona Uovu unazidi kuchipuka ndani ya kanisa, hapana nitasema.

Najua wengi watanichukia lakini sitaweza kunyamaza.

Yako mambo kadhaa ambayo nataka niyaseme kwa ukweli ambayo yanafanyika ndani ya Kanisa na kumdhalilisha Bwana Yesu. 

                 JAMBO LA KWANZA.

JE MUNGU ANAWEZA KUIPOKEA SADAKA YA MTU MWOVU?

Ni kweli kabisa kwamba Mungu Baba ndiye aliyeanzisha Utoaji Sadaka na ndiye kaweka utaratibu huu wa mwanadamu kutoa sadaka kwake.

Lakini pamoja na kwamba Mungu Baba ndiye katoa utaratibu wa mwanadamu kutoa sadaka kwake sio kila sadaka ambayo mwanadamu anaitoa Mungu anaipokea, au ataipokea hapana kabisa.
Leo hii kwenye Makanisa mengi na kwenye huduma za aina mbalimbali unasikia watu wakiambiwa toa sadaka toa sadaka na Mungu atakubariki na kukuinua Je ni kweli kabisa kila anayeitoa hiyo sadaka Mungu anaipokea? Jibu lake ni hapana.

Na mbaya zaidi watu hawafundishwi kuhusu sadaka gani ambazo Mungu hazipokei na sadaka zipi anazozipokea. Wanachotangaziwa na kulazimishwa kutoa tu sadaka.

Ngoja nikwambie ziko sadaka ambazo Mungu hawezi kuzipokea, kwa sababu Mungu ameweka utaratibu wake kuhusu Utoaji sadaka kwa mwanadamu na utaratibu huo uko ndani ya Neno lake Biblia.
Ngoja nikusomee mistari hii uone kitu ambacho Mungu anasema kwa habari ya sadaka.

                                           MITHALI 15

"8 Sadaka ya mtu MBAYA ni chukizo kwa BWANA......"

Unaona Sadaka anayotoa mtu mbaya ni chukizo mbele za Mungu yaani Mungu haipokei hiyo sadaka kabisa.

                                          MITHALI 21

"27 Sadaka ya wasio haki ni chukizo;........."

Unaona sadaka ya mtu asiye Haki akiitoa mbele za Mungu ni chukizo hiyo sadaka kwa maana kwamba Mungu haipokei hiyo sadaka.

                                                   AMOSI 5

"22 Naam, ijapokuwa mnanitolea sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka zenu za unga, SITAZIKUBALI; wala SITAZIANGALIA Sadaka zenu za amani, na za wanyama walionona".

Unamuona Mungu anasema hata kama mnatoa sadaka zenu yeye Hatazikubali na wala Hataziangalia kabisa kwanini?

Ziko sababAu kadhaa zinazomfanya Mungu asikubali na kuziangalia hizo sadaka na sababu mojawapo ni kwamba huyo anayeitoa hiyo sadaka ni mtu mbaya au mwenye dhambi.

Nimalizie kusema kwamba kama wewe ni mwenye dhambi na mtu mwovu ukimpelekea Mungu Sadaka zako hatazipokea kabisa uelewe hivyo.

Huyo mhubiri atapokea sadaka yako lakini Mungu hawezi kabisa kuipokea.
Je wewe sadaka zako unazotoa na kuambiwa na wahubiri utoe Mungu anazipokea au anazikataa na kutokuzikubali?

Ni lazima unapotoa Sadaka ufuate Kanuni na taratibu ambazo Mungu kaziweka ndani ya Neno lake zinazosimamia Utoaji sadaka.

Na sisi Wahubiri ni lazima tuwaambie Ukweli watu wanaotoa sadaka zao ili Mungu aweze kuzipokea sio tuwaambie tu toa toa toa sadaka wakati Mungu hatazipokea hizo sadaka zao. Tuiseme kweli ya Neno la Mungu kuhusu Utoaji sadaka.

Ni lazima unapompelekea Mungu Sadaka ni uwe umejitakasa kwa damu ya Yesu na uwe na Mahusiano mazuri na Bwana Yesu.

Tukutane wakati mwingine ambapo nitaendelea tena na ujumbe huu.

Peleka ujumbe huu kwa watu wengine.



                                    @Kibiriti 2017.
                                    

No comments:

Post a Comment

Featured Post

JINSI MISINGI YA VIZAZI INAVYOWEZA KUKAMATA MAISHA YAKO.

Fahamu kwamba misingi ni chanzo au asili au chimbuko la mtu. Na msingi wako wa vizazi unatokana na ukoo wako na kabila lako.      ...