Post Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 2, 2021

 Semina ya Siku 30 ( Christ For All People Church- Mbeya ).

KUYASHUGHULIKIA MALANGO YA KIROHO YANAYOGUSA MFUMO WAKO WA MAISHA YA KILA SIKU.

          Day 4 ya Semina.

Senior Pastor Samwel Kibiriti.

Shalom mwana wa Mungu karibu katika semina ya siku ya leo na Mungu atakuhudumia, leo tujifunze jambo hili kuhusu Malango.

JINSI MALANGO YANAVYOFANYA KAZI KIROHO KWAAJILI YA MAISHA YAKO.

Leo nataka nikuonyeshe jinsi malango ya kiroho yanavyofanya kazi kila siku kwaajili ya maisha yako na huu utendaji kazi wa malango upo katika ulimwengu wa roho, hivyo hakikisha kwamba unatafakari mambo haya ninayoenda kukufundisha na kuingia katika maombi;

               ANGALIA POINTI ZIFUATAZO:

( 1 ) Mungu ndiye aliyeumba malango ya kiroho.

Mwanzo 1:1 Wakolosai 1:16

🔵 Nataka utambue kwamba Mungu ndiye muumbaji wa kila kitu hivyo hata malango ya kiroho yameumbwa na Mungu na Mungu aliyaumba na kuyatengeneza malango kwa kusudi lake jema ili kuyatumia malango kukutana na maisha ya mwanadamu. Hivyo uelewe kwamba shetani hajawahi kuumba malango ya kiroho ila ni Mungu ndiye aliyeyaumba malango yote ya ulimwengu wa kiroho.

( 2 ) Dhambi ilipoingia ulimwenguni ilimpa uhalali shetani wa kutumia malango ya kiroho.

Warumi 5:12 Waefeso 4:27

Dhambi ilipoingia ulimwenguni ilisababisha madhara mengi sana na kati ya madhara hayo shetani alipata uhalali wa kuingia na kuyatumia malango ya kiroho ya mwanadamu. Kwahiyo leo hii watu wengi malango yao ya maisha yameshikiliwa na shetani na miungu na kujikuta wanateseka kwasababu shetani ameyashikilia hayo malango, hivyo unapofanya maombi ya malango ukumbuke kuanza maombi yako kwa toba ili upate msaada wa Mungu katika hayo malango.

( 3 ) Malango yapo katika ulimwengu wa kiroho lakini matokeo yake ya utendaji kazi huonekana katika ulimwengu wa mwili.

Waebrania 11:3  Isaya 60:11

Malango yapo kwenye ulimwengu wa roho lakini matokeo ya utendaji kazi wa hayo malango huonekana kwenye ulimwengu wa mwili wa maisha yako hivyo maisha unayoyaishi sasa hivi hapa duniani ni matokeoa ya kile kinachoendelea katika ulimwengu wa roho kwenye malango yako. Hakikisha kwamba unafanya maombi ya kupambana na roho zote zinazotengeneza matokeo mabaya katika maisha yako kupitia malango yako ya kiroho kwasababu usipopambana na hizo roho zitazidi kila siku kukutengenezea matokeo yao mabaya na kujikuta unaendelea kuishi maisha ya mateso hapa duniani.

( 4 ) Malango ya kiroho yanaweza kushikiliwa na maadui.

Kumbukumbu 28:52-53,57 

Malango yako ya kiroho au malango ya Familia na nchi na mji yanaweza kushikiliwa na maadui rohoni na malango mengi ya maisha yako yameshikiliwa na maadui rohoni. Leo kuna watu malango yao ya Uchumi na Ndoa na Kazi na Elimu na Biashara na Familia na Ndoto n.k yameshikiliwa rohoni na maadui zao na kujikuta wanazidi kuteseka katika hayo maeneo pasipo kupata mpenyo wowote wa kimaisha. Ingia kwenye ulimwengu wa roho na kuyafungua malango yako yaliyoshikiliwa na maadui ili uteseke kimaisha.

( 5 ) Malango ya kiroho yanakuwa na wasimamizi/walinzi.

2Samwel 18:24-27; 19:8 Ruthu 4:1-3 Esta 5:13 Waefeso 6:12 2Korintho 4:18

Malango yote katika ulimwengu wa roho yako na wasimamizi na walinzi ambao wanaweza kutoka kwenye ufalme wa Mungu au kutoka kwenye ufalme wa giza. Kazi ya walinzi ni kuhakikisha kwamba wanalinda hayo malango ili mtu mwingine asijekuyachukua, na kazi za wasimamizi wa malango ni kuhakikisha wanakusimamia au kuwasimamia katika maisha yenu ili muweze kuishi sawasawa na yale yaliyopangwa kupitia kwenye hayo malango yenu.

Na watu wengi ukifuatilia kwenye malango yao ya kiroho wamekaa wasimamizi na walinzi wa ufalme wa giza ambao ni mapepo na majini na wachawi na waganga wa kienyeji ili wahakikishe kwamba wanawatesa sana katika maisha yao. Hakikisha unaingia kwenye maombi kupambana na wasimamizi na walinzi wa malango yako ya kiroho kwasababu kama hutaweza kuwashinda hao hutaweza kutoka katika utumwa huo unaopitia leo ndio maaana pambana nao rohoni na uwashinde na kuwandoa katika malango yako kisha ruhusu Malaika wa Mungu ayalinde malango yako.

( 6 ) Malango yako na vichwa kiroho na kusikia yakisemeshwa.

Zaburi 24:7-10

🔴 Malango ya kiroho yako na vichwa na pia yako na uwezo wa kusikia kabisa yakisemeshwa ndio maana unaona hapo malango yanasemeshwa yainue vichwa vyao juu ili Yesu Kristo mfalme wa utukufu aweze kuingia. Hivyo unatakiwa sana kuombea vichwa vya malango yako ya kiroho kwasababu vikishambuliwa kuna madhara yake makubwa sana na hayo madhara utayaona kwenye maisha yako, pia hakikisha unayasemesha malango yako ya kiroho kila siku na kuachilia Neno la Mungu katika hayo malango yako.

( 7 ) Maadui na watesi wanaingia katika malango.

Maombolezo 4:12

🔵 Katika malango yako wanaweza kuingia maadui na watesi kwahiyo kama kwenye maisha yako kuna maadui wa aina mbalimbali wanaopambana nawe ujue kwamba waliingia kwenye malango yako ya kiroho. Unapoona maadui wanapambana nawe katika Ndoa yako au Uchumi wako au Elimu yako au Familia au Afya yako au kwenye Biashara yako utambue wazi kwamba hao maadui waliingia katika malango yako hayo ya ndoa, biashara, uchumi, elimu, familia, afya.

Siku zote nikuelewe jambo hili maadui wanapoingia na watesi katika malango yako ya kiroho au katika malango yenu ya nchi na mji na eneo na familia ujue kuna kazi maalum inayowaleta katika hayo malango kuifanya, hivyo hakikisha kwamba unaingia kwenye maombi na kupambana na maadui na watesi walioingia kwenye malango yako na kukutesa na kuziharibu kazi zao zote wanazozifanya ndani ya hayo malango kwaajili ya maisha yako na maisha yenu.

🔶 Kwa leo nimeweza kukufundisha ujue utendaji kazi wa malango kiroho ili unapofanya maombi ya kuombea malango ya maisha yako na malango ya maisha yenu uwe na Ufahamu wa Neno la Mungu, naamini kwamba somo hili limekujenga na kukupatia maarifa kuhusiana na wewe sasa kuingia kwenye maombi ya kuyaombea malango yako ya kiroho kuhusiana na maisha yako au maisha yenu. Ila kumbuka kabla hujaanza kupambana kwenye maombi ya malango kanuni yake omba toba mbele za Mungu kwaajili ya maisha yako pia utubu kwa Mungu kwaajili ya hayo malango unayoyaombea kisha ujiweke Wakfu kwa Mungu ndipo sasa uanze kufanya maombi yako ya malango.

✔️ Kwa leo tunaishia hapa katika semina yetu tukutane siku ya kesho ambapo nitaanza kukufundisha kuhusu Lango la Nchi unayoishi. Naomba unisaidie kuwashirikisha wengine na magroup mengine masomo haya ya semina ili watu wengi wapokee Maarifa haya ya Neno la Mungu.



Kwa Mawasiliano nami utanipata kwa namba hizi:

Vodacom +255 765 867574 ( WhatsApp ).

Airtel +255 785 855785.

Tigo +255 673 784197.

Kwa Email address ni Pastorkibiriti@gmail.com

Mimi ni Mwalimu wa Neno la Mungu la Maarifa

            Samwel Kibiriti.

Mei 18, 2021

Mbeya Tanzania.

@Kibiriti2021

( Semina hii ninaifundisha hapa Mkoani Mbeya katika Mji wa Uyole Kati, Karibuni wakazi wa Mbeya kila siku kuanzia saa 9-12 Jioni ).


No comments:

Post a Comment

Featured Post

JINSI MISINGI YA VIZAZI INAVYOWEZA KUKAMATA MAISHA YAKO.

Fahamu kwamba misingi ni chanzo au asili au chimbuko la mtu. Na msingi wako wa vizazi unatokana na ukoo wako na kabila lako.      ...