Post Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 3, 2021

 Semina ya siku 30 ( Christ For All People Church- Mbeya ).

KUYASHUGHULIKIA MALANGO YA KIROHO YANAYOGUSA MFUMO WAKO WA MAISHA YA KILA SIKU.

         Day 5 ya Semina.

Senior Pastor Samwel Kibiriti.

Bwana Yesu Kristo atukuzwe mwana wa Mungu karibu katika Semina ya siku ya leo ambapo tunataka kujifunza jambo hili;


KUPAMBANA NA LANGO LA NCHI UNAYOISHI ( A ).

Mathayo 12:40  Nahumu 3:13 Yona 1:8

Leo nataka tuanze safari ya kujifunza kuhusu lango la nchi unayoishi ambapo kuna mambo kadhaa nahitaji kusema nawe kwa siku 4 mfululilo. Kuna watu wengi maisha maisha yamefungwa kwenye malango ya nchi zao wanazoishi pia kuna nchi nyingi zinapitia katika mazingira magumu kutokana na yale yanayoendelea katika malango yao ya nchi, naamini kuna ufahamu mkubwa sana utaupata kupitia masomo haya.

MASWALI YA KUJIULIZA KUHUSU LANGO LA NCHI:

Kila nchi iko na malango yake kiroho na malango kati ya nchi na nchi yanatofautiana kwenye utendaji kazi wake, sasa nataka tujifunze somo hili kwa mfumo huu wa maswali, ambapo kila siku tutakuwa tunajifunza swali moja na kupata majibu yake, twende pamoja;

              SWALI LA KWANZA:


( 1 ) Je moyo wa nchi yenu unafanyaje kazi kiroho?.

         Mithali 4:23

🔴 Kila nchi iko na moyo wake kiroho sawasawa na Mathayo 12:40 sasa nataka nikuulize huo moyo wa nchi yenu unafanyaje kazi kiroho? Vile moyo wa nchi unavyofanya kazi matokeo yake yataonekana katika nchi na kwenye maisha ya wananchi. Watu wengi hawaombei moyo wa nchi kila siku kwasababu hawajui kiroho umuhimu na uzito wa moyo wa nchi. Sikiliza moyo wa nchi ndio Kiini cha uhai wa nchi, hivyo moyo wa nchi ukipata shida ujue kwamba nchi na nyie wananchi hamuwezi kukaa sawasawa.


( A ) Moyo wa nchi yenu umebeba mawazo na roho  za aina gani?.

Yeremia 4:14  Mathayo 15:19

🔵 Nataka nikuulize swali hili je katika moyo wa nchi yenu umebeba mawazo na roho za aina gani? Mawazo yaliyobebwa ndani ya moyo wa nchi ndio utakayoyaona yanafanya kazi kwa viongozi na wananchi pia roho iliyomo ndani ya moyo wa nchi yenu ujue kwamba ndio roho itakayotenda kazi katika nchi na mifumo yake, hivyo hizo roho sugu unazoziona katika nchi yenu ufahamu kwamba zimebebwa katika moyo wa nchi yenu hivyo ni lazima upambane nazo katika moyo wa nchi yenu na kuzing'oa hapo ndipo utaona hata katika nchi zinakosa nguvu.


( B ) Moyo wa nchi yenu imeshikiliwa na nani kiroho?.

1Wafalme 11:4  Mithali 21:1

Nani aliyeushikilia moyo wa nchi yenu kiroho? Mnaweza kuishi ndani ya nchi mkidhania moyo wa nchi yenu uko salama kumbe rohoni umeshikiliwa na shetani/miungu na mdhani kwamba nchi itakuwa na usalama na mafanikio hilo haliwezekani. Sababu mojawapo ya nchi nyingi kuteseka na wananchi kuishi maisha magumu kila siku ni kutokana na madhara ya moyo wa nchi kushikiliwa na miungu badala ya kushikiliwa na Mungu katika Yesu Kristo.

🔶 Sikiliza nikuambie yule aliyeshikilia moyo wa nchi yenu rohoni ndiye mwenye maamuzi ya nchi yenu iweze kwasababu moyo ndio kiini cha uhai wa nchi. Kanisa linatakiwa sana kuombea moyo wa nchi na kuukabidhi kwenye mikono ya Mungu aliye hai katika Yesu Kristo ili nchi na maisha ya wananchi yawe sawasawa na kusudi la Mungu lakini kanisa mkiendelea kulala na kudharau kuombea moyo wa nchi yenu na kushindwa kuutoa kwenye mikono ya miungu mtambue kwamba hamtaweza kufikia viwango ya maisha mlivyopangiwa na Mungu katika nchi pia nchi yenu itaendelea kupitia katika nyakati ngumu naza matatizo mbalimbali.


( C ) Moyo wa nchi umebeba vita ya aina gani kwaajili ya nchi?.

Hesabu 10:9  Isaya 40:2 Kutoka 17:14-16

Moyo wa nchi unabeba vita na kuna vita za aina tofauti tofauti zimebebwa katika moyo wa nchi na vita nyingine sio nzuri kubebwa katika moyo wa nchi kwasababu ziko na madhara makubwa kwa nchi na maisha ya wananchi ya kila siku.

✔️ Moyo wa nchi ukibeba vita ya kiuchumi utakuta katika nchi na wananchi wanapitia katika vita hiyo ya kiuchumi na  kufanikiwa kiuchumi.

✔️ Moyo wa nchi ukibeba vita ya magonjwa utakuta katika nchi na wananchi wanapambana sana na magonjwa ambayo yanawatesa bila kupata ufumbuzi wa kina. 

✔️ Moyo wa nchi ukibeba vita ya uchawi mtajikuta katika nchi na maisha ya wananchi mnateswa na kushambuliwa sana na roho hizo za uchawi katika maisha yenu.

✔️ Moyo wa nchi unaweza kubeba vita ya kukataa kusudi la Mungu hivyo utaiona nchi haisimami katika kusudi la Mungu na hata wananchi nao utawaona hawasimami katika kusudi lako la uumbaji kwasababu hiyo vita inawadhibiti kuhakikisha kwamba hawasimami katika lile kusudi la kuumbwa na Mungu na kuletwa hapa duniani.

❌Je moyo wa nchi yenu umebeba vita ya aina gani? Elewa kwamba vita iliyobebwa katika moyo wa nchi ndio utakayoiona ikiitesa nchi na kuwatesa wananchi kwenye maisha yao ya rohoni na mwilini, hivyo kanisa unatakiwa kupambana sana na vita iliyomo ndani ya nchi ambayo chanzo chake ni kuzimu na kuhakikisha kwamba nchi yenu haibebeshwi hizo vita za giza kwasababu zitawasumbua kizazi hadi kizazi katika nchi.


Tafakari Swali hili la Kwanza leo na hivyo vipengele 3 vilivyomo katika swali hilo na hakikisha unayafanyia kazi haya Mungu aliyosema nawe kuhusu moyo wa nchi unayoishi. Tukutane siku ya kesho ambapo nitakuuliza swali la Pili kuhusu Lango la nchi unayoishi, nakuomba washirikishe watu wengine na katika magroup mengine somo hili ili nao pia wapokee maarifa haya.



Kwa mawasiliano nami zaidi utanipata kwa namba hizi:

Vodacom +255 765 867574 ( WhatsApp ).

Airtel +255 785 855785.

Tigo +255 673 784197.

Kwa Email address ni Pastorkibiriti@gmail.com

Mimi ni Mwalimu wa Neno la Mungu la Maarifa

           Samwel Kibiriti.

Mei 19, 2021

Mbeya Tanzania.

@Kibiriti2021

( Semina hii ninaifundisha kanisani hapa mkoani Mbeya katika mji wa Uyole Kati, karibuni wakazi wa Mbeya kila siku kuanzia saa 9-12 Jioni ).

No comments:

Post a Comment

Featured Post

JINSI MISINGI YA VIZAZI INAVYOWEZA KUKAMATA MAISHA YAKO.

Fahamu kwamba misingi ni chanzo au asili au chimbuko la mtu. Na msingi wako wa vizazi unatokana na ukoo wako na kabila lako.      ...