Post Top Ad

Post Top Ad

Saturday, June 12, 2021

 Semina ya siku 30 ( Christ For All People Church-Mbeya ).

KUYASHUGHULIKIA MALANGO YA KIROHO YANAYOGUSA MFUMO WAKO WA MAISHA YA KILA SIKU.

        Day 9 ya Semina.

Senior Pastor Samwel Kibiriti.

Asifiwe Yesu Kristo rafiki yangu karibu katika semina ya siku ya leo.

KUPAMBANA NA MADHABAHU ZA NCHI ZILIZOFUNGA MAISHA YAKO NA MAISHA YENU ( B ).

Kumbukumbu la torati 12:1-4

Katika semina ya jana nilizungumza nawe mambo mawili kuhusu madhabahu za nchi zinavyohusika na maisha yako ndani ya nchi ya kila siku leo nataka nikuonyeshe mambo mengine twende pamoja.

UTENDAJI KAZI WA MADHABAHU ZA NCHI KUHUSU MAISHA YAKO YA KILA SIKU:

Tuangalie aina nyingine za huo utendaji kazi;


                  JAMBO LA TATU:

( 3 ) Madhabahu za nchi zinaweza kupitisha vita kwako inayotokana na makabila yaliyomo ndani ya nchi.

Yona 1:8 Ufunuo 13:1-2,7 Habakuki 3:9 Zekaria 11:10 Ufunuo 5:9

Kuna vita ndani ya nchi ambazo chanzo chake ni madhabahu za nchi kwa kutumia makabila yaliyomo ndani ya nchi yenu, kwahiyo swala la kujua idadi za makabila yaliyomo ndani ya nchi yenu na utendaji kazi wa hayo makabila ni jambo la msingi sana kulijua kiroho. Kwahiyo kuna vita kwenye maeneo mbalimbali ya maisha yako unazokutana nazo kila siku ambazo chanzo chake ni madhabahu za nchi kutumia makabila yaliyomo ndani ya nchi.

❌Je katika nchi unayoishi hizo madhabahu za miungu zilizomo ndani ya nchi zinatumia vita gani za makabila kuja kwenye maisha yako? Hakikisha kwamba unapambana kwenye maombi yako kupangua vita vyote unavyokutana navyo kutoka kwenye madhabahu za nchi kwasababu ya makabila yaliyomo ndani ya nchi.


                 JAMBO LA NNE:

( 4 ) Madhabahu za nchi zinaweza kuyafunga maisha yako kupitia viapo vinavyofanywa kwenye hizo madhabahu kwaajili ya nchi unayoishi.

1Waflme 8:31  Hesabu 30:2 Mathayo 23:20

🔵 Kuna watu wengi sana katika nchi maisha yao yamefungwa na viapo vilivyofanyika na vinavyofanyika ndani ya nchi kila siku kupitia madhabahu za nchi za miungu na viapo hivyo vinahusisha kuifunga nchi na kwasababu wewe unaishi ndani ya nchi unajikuta unadhurika na hivyo viapo vinavyofanyika kila siku kwa siri katika nchi yenu, kama hutakuwa mtu wa kuiombea nchi na kupambana na hizo madhabahu utajikuta maisha yako hayastawi ukiwa ndani ya nchi kutokana na hivyo viapo vya nchi.

❌Je unajifunguaga kila siku katika viapo vya madhabahu za nchi yenu? Hakikisha unapambana sana na viapo vya madhabahu za nchi yenu kila siku kwa maombi na kuyafungua maisha yako na maisha yenu ili uweze kuwa na maisha mazuri katika nchi unayoishi.


                  JAMBO LA TANO:

( 5 ) Sadaka zinazotolewa kwenye madhabahu za miungu za nchi yetu zinaweza kuyafunga maisha yako.

Ezra 3:2  Zaburi 118:27 Waamuzi 6:11,25-26

Kuna maisha ya watu ndani ya nchi yamefungwa na sadaka zilizotolewa kwenye madhabahu za nchi za miungu, na kuna watu wengi wanatoa sadaka kwenye madhabahu za nchi ili kuifunga nchi unayoishi na maisha ya nyie wananchi mliomo ndani ya nchi, hivyo hakikisha kwamba unapambana na jambo hili kwenye ulimwengu wa roho.

❌Je unafanya maombi ya kuharibu kila sadaka zilizotolewa kwenye madhabahu za miungu za nchi yenu zilizofunga maisha yako? Hakikisha unayafungua maisha yako kwenye hizo sadaka katika hizo madhabahu za nchi, pia hakikisha kwamba unakuwa mtiifu na mwaminifu katika kutoa Sadaka mbalimbali kwenye madhabahu ya Mungu katika Yesu Kristo kila wakati ili kupitia sadaka hizo unazotoa kwa Mungu hiyo madhabahu ya Mungu iweze kupambana na hizo madhabahu za nchi za miungu.

✔️ Tunaishia hapa kwa semina ya leo tukutane siku ya kesho ambapo tutaliangalia lango la Nafsi yako hakikisha kwamba unafanyia kazi somo hili kila siku kwa maombi yako. Nakuomba pia hakikisha unawashirikisha watu wengine na magroup mengine masomo haya ili wapokee Maarifa haya ya Neno la Mungu.


Kwa mawasiliano nami utanipata kwa namba hizi:

Vodacom +255 765 867574 ( WhatsApp ).

Airtel +255 785 855785

Tigo +255 673 784197

Kwa Email address ni Pastorkibiriti@gmail.com



Mimi ni Mwalimu wa Neno la Mungu la Maarifa

          Samwel Kibiriti.

Mei 23, 2021

@Kibiriti2021

Karibu upokee Maarifa mbalimbali kwenye Vitabu nilivyoandika vya Neno la Mungu.

No comments:

Post a Comment

Featured Post

JINSI MISINGI YA VIZAZI INAVYOWEZA KUKAMATA MAISHA YAKO.

Fahamu kwamba misingi ni chanzo au asili au chimbuko la mtu. Na msingi wako wa vizazi unatokana na ukoo wako na kabila lako.      ...