Post Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 23, 2021

 Semina ya siku 30 ( Christ For All People Church- Mbeya ).

KUYASHUGHULIKIA MALANGO YA KIROHO YANAYOGUSA MFUMO WAKO WA MAISHA YA KILA SIKU.

           Day 11 ya semina.

Senior Pastor Samwel Kibiriti.

Bwana Yesu Kristo asifiwe mwana wa Mungu napenda kukukaribisha katika semina ya leo, ambapo tunaendelea kujifunza kuhusu lango la Nafsi yako.

KUSHUGHULIKIA LANGO LA NAFSI YAKO ( B ).

Zaburi 25:20 Kutoka 32:7 Kumbukumbu 4:16 Hesabu 11:18 Zaburi 7:5 Hesabu 31:50

Katika Semina ya siku ya jana nilikufundisha kuhusu Sababu ya vita katika Nafsi yako ambapo nilikuonyesha sababu sababu sita za Kibiblia naamini umekuwa na maombi kuombea nafsi yako, leo naomba tusogee mbele kidogo nikufundishe jambo hili;

KWANINI NAFSI YAKO INASHAMBULIWA KWENYE ENEO LA AKILI?.

Nafsi za watu zinashambuliwa katika eneo la akili ndio maana kuna watu wengi akili zao zimepata madhara na kushindwa kufanya kazi kama Mungu alivyoziumba kwenye maisha yao, hapa nataka nikuonyeshe sababu kadhaa za kiroho ili uwe na umuhimu zaidi wa kuiombea nafsi yako na akili zako kila siku.


   JAMBO LA KWANZA:

( 1 )  Akili zako zinashambuliwa ili usiweze kuzitumia ipasavyo kama Mungu alivyotaka

1Wakorintho 15:34

Mungu amekupatia akili ili wewe uzitumie  kama ipasavyo lakini watu wengi hawatumii akili zao kama ipasavyo kwasababu zimeshambuliwa au kufungwa rohoni, kwahiyo Mungu anakutaka uweze kutumia akili zako kama ipasavyo maana yake kama alivyokusudia uzitumie sawa na kusudi lake la kukuwekea akili ndani yako. Kwahiyo shetani anashambulia akili zako ili ushindwe kuzitumia kama ipasavyo na usipozitumia kama ipasavyo kuna vitu utakosa kwenye maisha yako, Uwe mtu wa kukumbuka kuziombea akili zako kwasababu niza thamani sana katika maisha yako ya kila siku hapa duniani.


JAMBO LA PILI:

( 2 ) Akili zako zinashambuliwa ili kuchunguzwa vile vilivyobebwa ndani ya hizo akili

Isaya 40:28

Kwenye ulimwengu wa roho kuna mashetani ambayo huzichunguza akili za wanadamu ili kufunga vile vitu ambavyo Mungu kaibebesha hiyo akili ya mtu na kile anachotakiwa kufanya. Akili za Mungu hazichunguziki ninachotaka uone kwenye ulimwengu wa roho wanaweza kuzishambulia akili zako ili wazichunguze ndani yake na kuzishikilia, kwahiyo hakikisha kwamba unaombea akili zako na kuzifunika kwa damu ya Yesu ili zisichunguzwe na ziweze kutoa vile ilivyobebeshwa kwako na Mungu kwaajili ya maisha yako.

Kuna watu leo wanaishi maisha ya umasikini na magumu sana tofauti na mpango wa Mungu kwasababu akili zao zimefungwa kiroho ingawa Mungu alipowawekea akili zao kwenye nafsi akizibebesha hazina kubwa ya vitu vya thamani kwaajili ya maisha yao.


JAMBO LA TATU:

( 3 ) Akili zako zinashambuliwa ili wapate urahisi wa kuziloga.

Wagalatia 3:1-3

Wako watu wengi sana ambao akili zao zimelogwa rohoni ndio maana kuna vitu vya ajabu wanafanya kwenye maisha yao mpaka watu husema “ huyu kweli anazo akili zake kweli kwanini amefanya hivi?” akili anazo lakini bahati mbaya ni kwamba alishindwa kuzilinda na wachawi wamefanikiwa kuziloga ndio maana anafanya hayo anayoyafanya. Unawaona hawa Wagalatia ambao Mtume Paulo alikuwa anazungumza nao hapa walianza vizuri sana katika Roho lakini ghafula akili zao ziliposhambuliwa na kulogwa wakajikuta wanamuacha taratibu Yesu Kristo na kuanza kufuata matendo ya mwili. 

Akili za mtu zinaposhambuliwa na kulogwa lazima atabadilisha mwelekeo wake ataanza kwenda kinyume na alivyokuwa anaenda mwanzoni wakati akili zake hazijalogwa, na kuna matendo ambayo mwanzoni alikuwa hayafanyi ataanza kuyafanya yasiyokuwa mapenzi ya Mungu Kwahiyo atahitaji msaada kwa akili zake kufunguliwa na kukombolewa kwa jina la Yesu Kristo.


JAMBO LA NNE:

( 4 ) Akili zako zinashambuliwa ili usiweze kuzitumia katika mambo yote ya maisha yako

2Timotheo 2:7

Mungu amekupatia akili ili uweze kuzitumia katika mambo yako yote unayofanya kwenye maisha yako, lakini kunao watu ambao kwenye maeneo Fulani ya maisha yao hawatumii akili zao kufanya hayo mambo na matokeo yake hujikuta wanakosana na wenzao. Ni kusudi la Mungu kwamba utumie akili katika mambo yote lakini kwenye ulimwengu wa roho akili zako zinaposhambuliwa utajikuta huwezi kuzitumia katika mambo yote, na katika yale mambo ambayo hutatumia akili yako utajikuta unakosana na wenzako wale ambao wametumia akili zao kwenye hilo jambo. 


JAMBO LA TANO:

( 5 ) Akili zako zinashambuliwa ili zisiwe na Uwezo wa kuvumbua na kubuni  vitu vipya

Kutoka 35:30-35

🔴 Mungu ameweka uvumbuzi wa ajabu sana kwenye akili za  mwanadamu  na anatamani sisi wanadamu tuzitumie akili zetu kuvumbua vitu na kubuni  vitu alivyotukusudia lakini sivyo ilivyo kwenye maisha ya watu wengi huo  uwezo haufanyi  kazi tena kwenye akili zetu. Unaona jinsi hawa akina  Bezaleli na Oholiabu walivyotumia akili zao kuvumbua vitu na kufanya vile vitu ambavyo Mungu aliviweka kwenye akili zao. Katika akili  yako Mungu  ameweka vitu vya thamani sana na Uvumbuzi na  ujuzi wa  aina  mbalimbali je kiwango gani umeitumia akili yako ikafanya hivyo? 


JAMBO LA SITA:

( 6 ) Akili zako zinashambuliwa ili usiweze kuzitumia kama kiongozi.

Kumbukumbu 1:13-15  1Waflme 5:7

🔵 Kuna watu ambao wamewekewa uongozi ndani yao lakini akili zao kwasababu zimeshambuliwa wanajikuta hawafanyi vizuri kwenye nafasi zao za uongozi kwa sababu wanashindwa kuunganisha akili zao na nafasi zao za uongozi. Kwahiyo unatakiwa uzitumie vizuri akili zako kama kiongozi mahali ambapo Mungu amekuweka na kukupatia nafasi hiyo ya kuwaongoza wengine ili wasiulaumu uongozi wako. Pia mke ni kiongozi na mume nae ni kiongozi ndani ya familia yao hivyo akili za mmojawapo zikifungwa utamuona atashindwa kutimiza wajibu wake kama kiongozi wa familia na kusababisha migogoro na matatizo ndani ya familia yake.


JAMBO LA SABA:

( 7 ) Akili zako zinashambuliwa ili usiweze kuzitumia kujiwekea akiba ya maisha yako ya kesho.  

Mithali 30:24

🔵 Mungu ametupatia akili na anatutaka tuzitumie akili zetu ili kujiwekea akiba ya maisha yetu ya kesho katika vile anavyotujalia kuvipata tusiweze kuvitumia vyote bali akili ituongoze kuweka sehemu ya akiba ya kesho.                Unatakiwa utumie akili zako vizuri kujiwekea akiba kidogo kidogo kwaajili ya maisha yako ya baadae naya watoto wako, usile kila kitu unachopata bila kuweka kidogo akiba. 

🔶 Nimekuonyesha mambo hayo machache ili uone kwanini akili zako zinashambuliwa rohoni kupitia kwenye nafsi yako? Hivyo hakikisha kwamba unaingia kwenye maombi kuombea nafsi na akili zako wewe pamoja na kuwaombea watoto wako, wazazi wako, ndugu zako, mke&mume wake kwenye maeneo ya akili zao ndani ya nafsi ili akili zao ziweze kuwa huru hapo ndipo watazitumia ipasavyo katika maisha yao ya kila siku hapa duniani.

✔️ Kwa leo semina yetu inaishia hapa tukutane siku ya kesho, nakuomba unisaidie kuwashirikisha wengine masomo haya ili wapokee msaada wa Mungu kupitia semina hii kwaajili ya maisha yao.


Kwa mawasiliano nami utanipata kwa namba hizi, pia zitumie kutoa sadaka yako kwa Mungu kwaajili ya semina hii.

Vodacom M-PESA +255 765 867574 ( WhatsApp ).

Airtel Money +255 785 855785

Tigo Pesa +255 673 784197

Kwa Email address ni Pastorkibiriti@gmail.com



Mimi ni Mwalimu wa Neno la Mungu la Maarifa

             Samwel Kibiriti.

Mei 25, 2021

Mbeya Tanzania.

@Kibiriti2021

Kumbuka Bwana Yesu Kristo anarudi hakikisha kwamba umeyaandaa maisha yako kwa kuokoka na kuishi maisha matakatifu hapa duniani huku ukiendelea kuyafanya mapenzi yake Mungu kila siku.

No comments:

Post a Comment

Featured Post

JINSI MISINGI YA VIZAZI INAVYOWEZA KUKAMATA MAISHA YAKO.

Fahamu kwamba misingi ni chanzo au asili au chimbuko la mtu. Na msingi wako wa vizazi unatokana na ukoo wako na kabila lako.      ...