Post Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 9, 2021

 Semina ya siku 30 ( Christ For All People Church- Mbeya ).

KUYASHUGHULIKIA MALANGO YA KIROHO YANAYOGUSA MFUMO WAKO WA MAISHA YA KILA SIKU.

        Day 8 ya Semina

Senior Pastor Samwel Kibiriti.

Asifiwe Yesu Kristo mwana wa Mungu karibu tuungane katika semina ya siku ya leo. 

KUPAMBANA NA MADHABAHU ZA NCHI ZILIZOFUNGA MAISHA YAKO NA MAISHA YENU ( A ).

Kumbukumbu 12:1-4

Baada ya kumaliza kukuuliza maswali 5 kuhusu lango la nchi unayoishi na kukuongoza jinsi ya kuomba kuhusiana na nchi yenu naamini kwamba umefanyia kazi yale maswali, leo na kesho nataka nikupitishe katika jambo hili la madhabahu za nchi jinsi zilivyohusika kuyafunga maisha yako. Kuna mamilion ya wananchi waliomo ndani ya nchi ambao maisha yao yamefungwa katika madhabahu zilizomo ndani ya nchi.


Madhabahu za nchi zimehusika sana kuyakamata na kuyafunga maisha ya watu waliomo ndani ya nchi kwasababu unapoishi katika nchi kiroho hizo madhabahu ziko na uhalali kukukamata na kukufunga kama hutajua jinsi ya kuomba. Na nchi nyingi duniani zimebeba madhabahu za miungu wala sio madhabahu za Mungu aliye hai katika Yesu Kristo, na kwasababu wakristo wameshindwa kumjengea Mungu madhabahu kila mahali wanapoishi na kufanya kazi wamejikuta maisha yao ya kila siku yanadhibitiwa kiroho na hizo madhabahu za nchi wanazoishi.


Wewe mwenyewe ni shahidi kuna mambo mengi sana kwenye maisha yako hayaendi vile unavyotamani na vile Mungu alivyokukusudia yaende kwasababu ya hizo madhabahu za nchi, unafanya kazi, unalima, unafuga mifugo, unasoma n.k lakini ukifanya tathimini unakuta mambo hayaendi kwa haraka yanaenda taratibu sana hadi ulazimishe sana kwa maombi, hivyo tambua kwamba kuishi katika nchi yenye madhabahu za miungu utapata shida sana katika maisha yako ya kila siku.

UTENDAJI KAZI WA MADHABAHU ZA NCHI KUHUSU MAISHA YAKO YA KILA SIKU:


Ngoja nikuonyeshe mambo machache ya kiroho kuhusu utendaji kazi wa madhabahu za nchi zinavyohusika na kuyakamata na kuyafunga na kuyaharibu maisha yako. Na kwasababu wakristo wengi hawana mahusiano mazuri na madhabahu ya Mungu ila wako na mahusiano mazuri na majengo yao ya makanisa wamejikuta watu wa kushambuliwa kimaisha na madhabahu za miungu za nchi pasipo kupata msaada mkubwa sana kutoka  kwenye madhabahu ya Mungu katika Yesu Kristo.


                 JAMBO LA KWANZA:

( 1 ) Madhabahu za nchi zinahusika na kazi zako unazofanya ndani ya nchi.

Zaburi 104:23 Waamuzi 6:11-32 Mhubiri 3:13,22 Ufunuo 16:7


Nataka utambue kwamba madhabahu za nchi unayoishi kiroho zinahusika sana na kazi zako za mikono unazozifanya ndani ya nchi pia na kazi zenu mnazozifanya ndani ya nchi na jambo hili watu wengi mnaoishi katika nchi hamlitambui lakini huo ndio ukweli kazi zako unazofanya ndani ya nchi zimeshikiliwa kiroho na madhabahu za miungu zilizomo ndani ya nchi yenu ndio maana hakuna faida kubwa unayoipata katika kazi zako za mikono ila unaendelea kufanya kwasababu huna namna yoyote ya kuishi usipozifanya hata kama haupati faida inayoshahili.


Wako watu wengi ndani ya nchi kazi zao za mikono wanazofanya kila siku zimeshikiliwa na kufungwa na madhabahu za nchi walizomo na hivyo kusababisha badala ya kazi kuwa sehemu ya furaha kwao kazi zimegeuka na kuwa utumwa kwao ndio unasikia mtu akisema hii kazi inanichosha sana au hii kazi sioni faida yoyote ya kufanya pamoja na kuajiliwa kwangu au hii kazi inajitesa tu ingawa naifanya. Haya yote yanasababishwa na utendaji kazi wa hizo madhabahu zilizomo ndani ya nchi yenu.


❌ Je madhabahu za nchi yenu zimehusika kwa kiwango gani kukutesa katika kazi zako za mikono? Hakikisha unaingia katika maombi ya nguvu kuzishughulikia madhabahu za nchi za miungu zilizofunga kazi zako za mikono unazozifanya ndani ya nchi kisha fungua kazi zako za mikono katika hiyo nchi na baada ya hapo hakikisha eneo unalofanyia kazi zako za mikono unamjengea Mungu Madhabahu yake hapo na kuziunganisha kazi zako za mikono na madhabahu ya Mungu aliye hai katika Yesu Kristo ndipo utaona faida na kustawi kwako kimaisha kupitia hizo kazi za mikono unazofanya katika nchi.


              JAMBO LA PILI:

( 2 ) Madhabahu za nchi zinaweza kukudhibiti katika kuliishi na kulitumikia Kusudi lako la Maisha.

Warumi 9:11, Waefeso 1:4 Mwanzo 11:31-32, 12:1-4


🔵 Katika nchi unayoishi nataka ujue kwamba hizo madhabahu za nchi yenu za miungu katika ulimwengu wa roho zimehusika kwa asilimia kubwa sana kukudhibiti katika kuliishi na kulitumikia kusudi la Mungu la kukuumba wewe na kukuleta hapa duniani, ndio maana angalia katika maisha yako kama uaishi ndani ya kusudi lako la uumbaji. Watu wengi ndani ya nchi hawako kwenye kusudi lao la uumbaji ila wanaishi maisha wakiwa nje ya kusudi ndio maana kilio cha maisha kuwa magumu hakiishi katika vinywa vyao.


Maisha yako Mungu alipokuumba aliyafunga ndani ya kusudi lako la uumbaji na alipokuleta hapa duniani Mungu amekusudia uweze kuyaishi hayo maisha yako kwa kipindi utakachokuwepo duniani ila kwa bahati mbaya kuna mambo mengi yemehusika kulishika kusudi lako yakiwepo madhabahu ya nchi unayoishi ndio sasa badala ya kuyaishi maisha yako halisi leo unaishi maisha photocopy yasiyokuwa yako ndio hapo sasa kuteseka na kuhangaika kumekuwa sehemu ya maisha yako kwasababu uko nje ya kusudi lako la kuumbwa na Mungu.


❌ Je madhabahu za nchi yako unayoishi zimeshikilia kusudi lako la kuumbwa na Mungu kwa kiwango gani? Je unaishi na kulitumikia kusudi la Mungu kwenye maisha yako ndani ya nchi uliyopo? Hakikisha unaingia kwenye maombi ya nguvu katika kuzipiga madhabahu zote za nchi za miungu zilizoshikilia kusudi lako la uumbaji, ziamuru zikuachilie na kuachia kusudi lako na pia hakikisha unalifungua kusudi lako la uumbaji kwenye hizo madhabahu za nchi, na kusudi la uumbaji la watoto na wazazi wako lifungue kwa damu ya Yesu na jina la Yesu Kristo katika nchi.


Kufahamu mambo mengi kuhusu Kusudi lako la uumbaji tafuta kitabu changu nilichoandika kiitwacho VITU VILIVYOBEBWA NDANI YA KUSUDI LAKO LA KUUBWA NA MUNGU ndani ya vitabu nimefundisha maarifa makubwa sana kuhusu kusudi ni Tsh 5,000 ( Elfu Tano ) karibu ujipatie Nakala yako.


✔️ Kwa leo semina yetu inaishia hapa tukutane siku ya kesho ya semina ambapo nitakuonyesha utendaji mwingine wa madhabahu za nchi unayoishi kuhusu maisha yako ya kila siku katika hiyo nchi. Nakuomba sana nisaidie kuwashirikisha watu wengine masomo haya na Mungu atakubariki kwa kuifanya huduma hii ili watu wengi wasiendelee kuteseka wapokee maarifa haya ya Neno la Mungu, ulitume somo kama lilivyo bila kuondoa chochote.


Kwa mawasiliano nami utanipata kwa namba hizi:

Vodacom +255 765 867574 ( WhatsApp ).

Airtel +255 785 855785

Tigo +255 673 784197

Kwa Email address ni Pastorkibiriti@gmail.com



Mimi ni Mwalimu wa Neno la Mungu la Maarifa

         Samwel Kibiriti.

Mei 22, 2021

@Kibiriti2021

Tukutane katika semina ya siku ya kesho ambapo Mungu atatuhudumia tena kama alivyokuhudumia siku ya leo.

No comments:

Post a Comment

Featured Post

JINSI MISINGI YA VIZAZI INAVYOWEZA KUKAMATA MAISHA YAKO.

Fahamu kwamba misingi ni chanzo au asili au chimbuko la mtu. Na msingi wako wa vizazi unatokana na ukoo wako na kabila lako.      ...